KUSULIBISHA MACHO

NENO LA LEO: FAIDA YA KUSULUBISHA MACHO

Mathayo 18:9 "Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanamu ya moto."

Mtume Paulo anatoa tafsiri ya Ukristo halisi, au wokovu halisi kuwa ni Kuusulibisha mwili wa dhambi na kufufuka na mwili mpya katika Kristo. Warumi 6:6 "mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;" Soma pia Wagalatia 2:20 "Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; ...."

Watu wengi wanadai ni wakristo, au wameokoka, au wacha Mungu, wakati ki uhalisia, bado viungo vyao viko hai katika dhambi. Leo tunaangalia kiungo cha MACHO. Kila tamaa mbaya inatokana na macho, macho ni kati ya kiungo ambacho kinatumiwa na shetani kuwatenga Watu na Mungu wao, kwa kuwaingiza kwenye dhambi.

Kwa kutazama tunabadilika, umezoea kutazama nini; ndivyo tabia yako inaumbika. Mfalme Daudi aliingiwa na pepo la zinaa alipomuangalia mke wa Uria akiwa uchi akioga, hadi akazini naye ... 2Samweli 11:2-4, Daudi akajitenga na Mungu kwa tendo hilo dakika chache tu. Hata leo wengi wamenasa na pepo la Zinaa na Uasherati, bila kisahau WIZI, WIVU, Tamaa mbaya n.k. kwa sababu ya kiungo MACHO.

Macho yanayotazama picha za Ngono au Ponograph, mabinti wanaotembea huku sehemu za siri zikiwa nje nje kama wanyama, Mabinti wanaotazama kwa kuzungusha macho utafikiri ya kinyonga, wanaotembea kwa kubinua na kuzungusha makalio utafikiri tairi za isuzu, yote hayo ni mitego ya KUNASA MACHO yasiyosulibiwa yapagawe na roho chafu za ngono.

Daudi alikili akisema "Sitaweka mbele ya macho yangu neno la uovu" - Zaburi 101:3, na baadaye alipoona yeye kwa akili yake hawezi akasema "Unigeuze macho yangu NISITAZAME visivyofaa, unihuishe katika njia yako" Zaburi 119:37. Wachungaji, manabii, watumishi na wapendwa, wengi wamenasa kwa KOPE za wadada, kama Sulemani anavyo onya - Mithali 6:25. "Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake."

Wapendwa marafiki zangu, tunaweza kushinda uovu wote utokanao na TAMAA ya macho, kwa kuamua kusulubisha kiungo hiki MACHO, yaani kuyasalimisha macho kwa Kristo, ili yafe kwa tamaa ya mwili na yahuishwe kwa mambo matakatifu chini ya utawala wa Roho matakatifu. Hebu kila mmoja ajiulize, macho yake yanatazama nini? kama yanapenda UOVU huo ni mtego wa adui umeshanasa.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi (+255 0766 992 265)
www.mwangosi. com

Previous
Next Post »